SHABIKI WA ZANZIBAR HEROES AWAOMBA RADHI WATANZANIA BARA

Na Said Ally
Shabiki wa Zanzibar Heroes ambae video yake ilisambaa katika mitandao mbalimbali ikionyesha namna alivyotoa lugha ya kejeli (matusi) kwa watanzania bara baada ya timu ya Zanzibar Heroes kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kilimanjaro Stars, leo hii ameomba radhi kwa kitendo hicho ambacho alikifanya.

Shabiki huyo alisema kwamba yeye hakufikilia kama jambo hilo ambalo amelifanya lingepokelewa vibaya na wadau wengi.

Alisema kwamba jambo hilo alilifanya kutokana na furaha aliyokuwa nayo kwa siku ile hasa baada Zanzibar Heroes kuchomoza na ushindi katika ushiriki wa michuano ya kombe la Challenge lakini halikuwa lengo lake kufanya vile.


No comments