TANZANIA YAZIDI KUPOROMOKA KWENYE VIWANGO VYA FIFA

Tanzania imeendelea kushuka katika viwango vya ubora ambavyo hutolewa na FIFA baada ya kushuka kwa nafasi tano katika mwezi novemba.

Kwa mujibu wa taarifa ya FIFA,kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 147 ikishuka kwa nafasi tano kutoka ile ya 142 ya mwezi Octoba.

Uganda wameendelea kutamba katika ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kuendelea kushika namba moja katika ukanda huo huku ikishika nafasi ya 75 duniani.

Kenya kwa upande wao wamepanda kwa nafasi tano wakishika nafasi ya 106 duniani huku Rwanda nao wakipanda kwa nafasi saba wakishika namba 113 duniani.

Burundi imeshuka kwa nafasi nne kutoka namba 138 hadi 142.

Senegal imeendelea kushika namba moja Afrika ikiwa nafasi ya 23 kwa FIFA ikifuatiwa na Tunisia katika nafasi ya pili huku ikiwa namba 27 duniani.

Nafasi ya tatu kwa Afrika imeshikwa na Misri ikiwa namba 31 kwa FIFA.

No comments