MOHAMED DEWJ AMTAKA JOSEPH OMOG ABWAGE MANYANGA

Na,Said Ally
Mwanachama wa klabu ya Simba,Mohamed Dewj maarufu kwa jina la MO,amemtaka kocha mkuu wa klabu hiyo Joseph Omog ajiuzulu.

Kupitia ukurasa wake wa instagramu MO,ameandika ujumbe wenye lengo la kushinikiza kocha huyo aweze kuachia ngazi katika majukumu yake ya ufundishaji ndani ya klabu ya Simba.

Kwa kuwa bado sina mamlaka ya maamuzi kwenye klabu ya Simba,kama mwanachama na mshabiki wa Simba,namuomba Omog kwa heshima na taadhima ajiuzulu"aliandika MO kupitia ukurasa wake wa instagram.

Huenda uamuzi huo wa MO umekuja baada ya klabu ya Simba kutolewa katika michuano ya kombe la FA na timu ya Green Worriers ambayo inashiriki ligi daraja la pili baada ya kufungwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-3 hapo jana.

Dewj ni mwanachama maarufu wa klabu hiyo ya Simba ambae ameshinda tenda ya uwekezaji ndani ya klabu hiyo kuelekea katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa timu.

No comments