TFF WASEMA MTANDAO WA TMS UKO VIZURI

Na Said Ally
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kuanzia leo hii vilabu vinapaswa kukamilisha taratibu za usajili kupitia mfumo wa mtandao baada mfumo huo kurejea katika hali ya awali.

Dirisha dogo la usajili lilifungwa rasmi siku ya tarehe 15 ya mwezi desemba lakini vilabu vilishindwa kuwasilisha majina ya wachezaji katika mfumo wa mtandao (TMS) kutokana na mtandao huo kufeli.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas alisema kwamba shirikisho hilo linaendelea kuvisisitizia vilabu kuwa mwisho wa kukamilisha zoezi hilo ni tarehe 23 mwezi huu na hakutakuwa na muda wa nyngeza.

No comments