NANDY AKILI KUANDIKIWA NYIMBO YA KIVURUGE

Na,Kilian Tz
Msanii wa bongo fleva anaeongelewa sana kwenye media tofauti hapa nchin kwa kipindi hiki 'Nandy"amekili kuandikiwa,,nyimbo yake inayofahamika kwa jina la kivuruge.

Nandy alikiri kuinunua nyimbo hiyo  baada ya kuulizwa gharama alizotumia katika wimbo huo lakini kwa mtazamo tofauti alishindwa kuitaja.

Alisema kwamba yeye alipendezwa na wimbo huo baada ya kuusikia akiwa studio hivyo akaamua kuomba auziwe wimbo huo wa Kivuruge ambao kwa sasa ni miongoni mwa ngoma zinazofanya vizuri katika soko la muziki.
Katika hatua nyingine Nandy amewahaidi mashabiki zake mambo mazuri katika mwaka wa 2018 akiamini utakuwa mwaka wa mafanikio zaidi kwa upande wake.

Mkali huyo wa bongo Freva hadi sasa hajafanya collabo na msanii yeyote zaidi ya remix ya nyimbo yake ya na gusa gusa ambapo amedai kuwa sababu inayopelekea kufanya hivyo ni kutokana na management yake ambayo inataka kuangalia uwezo wake akiwa pekee.

Aidha alisema kwamba wadau wake wategemee mambo mazuri mwaka 2018 huku akitarajia kufanya collaboration za wasanii kutoka nchi za nje na pia ujio wa album yake.

Nandy ni msanii aliyepata mafanikio makubwa katika mwaka huu wa 2017 hasa baada ya kupokelewa vyema na wadau wa mziki huku pia akifanikiwa kubeba tuzo ya msanii bora wa kike kwa Afrika "Afrima".

No comments