WAZIRI WA MICHEZO ZANZIBAR AINGILIA KATI SWALA LA WACHEZAJI WA TANZANIA BARA

Na Sleiman Ussi,Zanzibar
Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Rashid Ali Juma amewataka wachezaji waliopo katika timu ya taifa ya Zanzibar ( Zanzibar Heroes) kujituma kwa moyo wao wote ili kuviletea heshima visiwa vya Zanzibar.

Waziri Rashid ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari leo hii alipotembelea mazoezi ya timu hiyo katika kiwanja cha Amani mjini Unguja.

Mbali na swala hilo pia Rashidi ameahidi kuzitatu baadhi ya changamoto zinazoikabili timu hiyo ya Zanzibar hasa swala la kutowasili kwa wachezaji wanaotokea Tanzania bara.
Alisema kwamba kwa sasa ameshafanya jitihada za kuzungumza na wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo iliyo chini waziri Harrison Mwakyembe juu ya swala hilo ambapo kila kitu kinakwenda vizuri na anaamini wachezaji hao watawasili Zanzibar kwa wakati.


Kocha wa Zanzibar Heroes Hemed Morocco alisema kuwa ikifika Novemba 15 ikiwa bado wachezaji hao hawajawasili Zanzibar katika kambi ya timu hiyo atalazimika kuwaacha na kuongeza nguvu kwa vijana wanaocheza vilabu vya Zanzibar kwani hawawezi kuwaruhusu wachezaji hao kujiunga na kambi siku chache kabla hawajasafiri. 

No comments