KOCHA ZANZIBAR HEROES AAMUA KUACHANA NA WACHEZAJI WA TANZANIA BARA

Na Sleiman Ussi,Zanzibar
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), ambao wapo katika ligi kuu soka Tanzania bara huenda wakaachwa katika kikosi hicho kutokana na kutopewa ruhusa na vilabu vyao kujiunga na timu hiyo ya Taifa mpaka ligi kuu bara itakapokwenda mapumziko.

Kocha mkuu wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman (Morocco) ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba kutokana na kutopewa ruhusa wachezaji hao huenda wakawasamehe na badala yake atawachagua wachezaji wengine wanaocheza ligi kuu soka hapa hapa Zanzibar.

Morocco alisema kuwa ikifika Novemba 15 ikiwa bado wachezaji hao hawajawasili zanzibar katika kambi ya Heroes watalazimika kuwaacha na kuongeza nguvu kwa vijana wanaocheza vilabu vya Zanzibar kwani hawawezi kuwaruhusu wachezaji hao kujiunga na kambi siku chache kabla hawajasafiri. 

"Tumeshaanza mazoezi tangu juzi, lakini uhakika wa kuwapata wachezaji wanaocheza ligi ya bara ngumu, tumewasiliana na vilabu vyao lakini wametuambia wachezaji hawatawaruhusu kujiunga na sisi mpaka ligi isimame Novemba 19, na sisi tunataka wachezaji wote walipoti kambini mapema ili tukiandae kikosi kwa ajili ya michuano ya Challenge"alisema Morocco.

No comments