AZAM FC WAMTUPIA VILAGO YAHAYA MOHAMMED

Uongozi wa klabu ya Azam FC,umetangaza rasmi kuachana na mchezaji Yahaya Mohammed baada ya benchi la ufundi na uongozi wa klabu kuafikiana maamuzi ya kutoendelea nae katika timu.

Afisa Habari wa Azam FC,Jafary Idd alisema kwamba kuanzia leo hii Yahaya Mohammed kutoka nchini Ghana si mchezaji wa timu hiyo hivyo milango iko wazi kwa timu zitakazomuhitaji.

Jafari alisema kwamba uongozi umechukua jukumu la kuachana na mchezaji huyo kutokana kutoridhishwa na kiwango chake licha ya kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wametoa mchango mkubwa kwa klabu ya Azam FC.

Hata hivyo Jafari aliongeza kwa kusema kwamba leo hii Yahaya anatarajiwa kuondoka kwa ajili ya kurejea nchini kwao Ghana.

No comments