KAULI YA YANGA JUU YA TAARIFA ZA LWANDAMINA KUJIUNGA NA ZESCO

Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Yanga umekanusha taarifa zinazoelezwa na baadhi ya wadau wa soka kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo George Lwandamina yuko mbioni kuachana na Yanga ili ajiunge na klabu yake ya zamani ya Zesco United ya nchini Zambia.

Afisa Habari wa timu hiyo Dismas Ten amesema kwamba,uongozi unatambua kuwa Lwandamina yuko kwao Zambia baada ya kupatwa na msiba na anatarajiwa kurejea hapa nchini siku ya jumatatu ya wiki ijayo kwa ajili ya kuendelea kukinoa kikosi cha timu hiyo.

Dismas aliongeza kwa kusema kwamba mashabiki wanapaswa kufahamu kuwa Lwandamina bado ni mwajiriwa wa klabu ya Yanga hivyo hawapaswi kuziamini taarifa za mitandaoni ambazo hazijathibitshwa na uongozi.

No comments