ZILIPENDWA YA WCB YALETA KIZAA ZAA

Na Said Ally
Baada ya Bendi ya Msondo Ngoma kupitia wanasheria wao kuwaandika wasafi (WCB) kuwadai jumla ya tsh 300M kutokana na wimbo wa "Zilipendwa" kwenye dakika ya 4:55-5:10 kuwa na mlio wa saxaphone ambao unafanana na uliotumika kwenye wimbo wa "Ajali" wa Msondo Ngoma (dak 6:38-7:6:52) bila kupata ruksa kinyume na sheria ya hatimiliki wadau mbalimbali wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya jambo hilo.

Baadhi ya wadau hasa kupitia kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kukasilishwa na kitendo hicho kilichofanywa na bendi ya Msondo wakidai hawakupaswa kufanya  hivyo.

Mbali na hao wanaopingana na bendi ya Msondo lakini wapo wengeine ambao wameiunga mkono bendi hiyo wakiwaamini wametumia haki yao ya msingi,kwani WCB ilishindwa kutumia uungwana wa kuomba matumizi ya mlio huo wa saxaphone.

Hata hivyo kwa mujibu wa barua inayosambaa mitandaoni inaeleza kuwa Msondo imetoa Siku 7 iwe imelipwa fedha hizo vinginevyo hatua zaidi za kisheria zitachukukiwa tena kwa Gharama zao WCB.

No comments