GEORGE LWANDAMINA AREJEA KWAO ZAMBIA

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba programu za timu hiyo zinataraji kuendelea siku ya kesho kwa ajili ya kujiwinda na michezo yao ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Msemaji wa timu ya Yanga,Dismas Ten alisema kwamba baada ya kurejea jijini Dar es salaam wakitokea mkoani Singida, siku ya kesho kikosi kitaanza mazoezi chini ya kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa.

Dismas alisema kwamba kikosi kitaongozwa na Nsajigwa baada ya kocha mkuu George Lwandamina kurejea Zambia kutokana na matatizo ya kifamilia.

Hata hivyo aliongeza kuwa wachezaji ambao wameitwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars tayari wamewapa ruhusa ya kuingia kambini katika timu hiyo inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin hapo novemba 12 mwaka huu.

No comments