SIMBA YAREJEA KILELENI KATIKA MSIMAMO WA LIGI

Timu ya Simba imefanikiwa kurejea kileleni katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara baada ya leo hii kufanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya bao 1-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Bao la ushindi katika mchezo huo limefungwa na winga hatari wa timu hiyo Shiza Ramadhani Kichuya kunako dakika ya saba ya mchezo akitumia uzembe uliofanywa na mabeki wa timu ya Mbeya City waliyezani ameotea baada ya kupokea mpira uliochongwa na Jonas Mkude.

Kwa matokeo matokeo hayo ambayo wameyapata timu ya soka ya Simba yanawafanya kurejea kileleni katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa kufanikiwa kufikisha alama 19 sawa na Azam FC,lakini Simba inaongoza kutokana na uwiano mzuri wa mabao ya kushinda.


No comments