YANGA YAKUMBANA NA RUNGU LA BODI YA LIGI

Klabu ya Yanga imepigwa faini ya shilingi laki 500,000/ na bodi ya ligi kutokana na sababu za mashabiki wake kurusha chupa uwanjani katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Simba iliyochezwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniphace Wambura amesema kwamba adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 42 kanuni ndogo ya kwanza kuhusu udhibiti wa klabu.

Katika mechi hiyo iliyochezwa octoba 28,timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

No comments