TAIFA STARS YAANZA MAZOEZI RASMI

Na Said Ally
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo hii kimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya Benin.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT.COM kwamba asilimia kubwa ya wachezaji tayari wamesharipoti kambini kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa tarehe 12 mwezi novemba mwaka huu.
Lucas alisema kwamba mchezaji Simon Msuva tayari amesharipoti kambini na leo hii ni miongoni mwa wachezaji waliofanya mazoezi katika uwanja wa JK Park.

Alisema kwamba kikosi hicho kinataraji kuelekea nchini Benin siku ya tarehe 9 tayari kwa pambano hilo ambalo kama Stars itashinda basi itajiweka kwenye mazingira mazuri ya kupanda kwenye viwango vya ubora vinavyotolewa na FIFA.

No comments