SAFARI NDEMLA KWENDA SWEDEN YAOTA MBAWA

Uongozi wa klabu ya Simba umesema kuwa  safari ya mchezaji Hamis Said Juma Ndemla iliyokuwa ifanyike leo Jumanne imesogezwa mbele.

Mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba,Haji Manara amesema kwamba Ndemla ambaye amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini Sweden ,sasa ataondoka nchini siku ya Alhamis ya tarehe 9 ya mwezi huu.

Manara alisema kwamba Mabadiliko hayo ya safari hayataathiri muda wake wa majaribio katika klabu hiyo,ambapo atakuwa huko kwa siku 14.

No comments