LULU DIVA ATAMBA KUENDELEA KUFANYA VYEMA

Msanii anaekuja kwa kasi katika muziki wa bongo Flava "Lulu Diva" ametamba kuendelea kufanya vizuri katika soko la muziki huo kutokana na jitihada ambazo anaendelea kuzifanya.
Mkali huyo anaetamba na nyimbo yake ya Give It To Me amesema kwamba bado ana chachu ya kuendelea kufanya vizuri hapa nyumbani na nje ya mipaka ya Tanzania ili kuitangaza vyema nchi kupitia kipaji chake.

Lulu ni miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri hivi sasa kutokana na ubora wa nyimbo zake pamoja na uwezo wa kumiliki jukwaa pale anapokuwa stejini.

Miongoni mwa ngoma ambayo ilimtambulisha Lulu Diva ni ile inayojulikana kwa jina la Usimwache ambayo ilipokelewa vizuri na wadau wa mziki kisha akaachia ngoma nyingine inayojulikana kwa jina la Utamu ambayo ni miongoni mwa wimbo unaotamba sana kwenye vituo vya radio na Tv kabla ya huu wa sasa wa Give It To Me uliothibitisha kipaji chake.

No comments