MSUVA AIPA NAFASI YANGA KUBEBA UBINGWA

Winga wa zamani wa timu ya soka ya Yanga ambae kwa sasa anakipiga katika klabu ya Difaa Hassan EL Jadidi  Simon Msuva ameipa nafasi kubwa timu yake hiyo ya zamani kuchukuwa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu.

Msuva ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT,kwamba licha ya klabu hiyo kuanza kwa kusua sua lakini anaamini kutokana na ubora wa kikosi cha timu hiyo nafasi ya kuchukuwa ubingwa ni kubwa kwa upande wao.

Alisema kwamba ligi ya msimu huu ina ushindani wa hali ya juu kutokana na ubora wa timu zote hasa baada ya kufanya maandalizi mazuri kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments