MSUVA AMPA NAFASI NDEMLA KUCHEZA SOKA LA KULIPWA

Winga wa zamani wa timu ya soka ya Yanga ambae kwa sasa anakipiga katika klabu ya Difaa Hassan EL Jadidi  Simon Msuva amesema kwamba mchezaji Said Hamis (Ndemla) ana nafasi kubwa ya kufanikiwa kufuzu kwenye majaribio yake ya kucheza soka la kulipwa nchini Sweden.

Msuva ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT,kwamba kutokana na uwezo aliokuwa nao mchezaji huyo wa wekundu wa Msimbazi Simba anaamini atafanikiwa katika majaribio hayo ya siku 14.

Ndemla ameelekea leo hii huko nchini Sweden kwa ajili ya kuanza kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini humo baada ya kupewa idhini na uongozi wa klabu ya Simba.

No comments