CROATIA YAICHAKAZA UGIRIKI

Timu ya taifa ya Croatia imepata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ugiriki katika mchezo wa mtoano wa mkondo wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia.

Magoli ya Croatia yamefungwa na Luka Modric kwa mkwaju wa penati, Nikola Kalinic akaongeza goli la pili,nae mshambuliaji Ivan Perisic akaongeza goli la tatu.

Mshambuliaji Andrej Kramaric akahitimisha kazi kwa goli la nne na  goli pekee la Urigiki katika mchezo huo limefungwa na Sokratis Papastathopoulos

Switzerland wakicheza ugenini wamewafunga Ireland Kaskazini kwa bao 1-0 bao ambalo limefungwa kwa mkwaju wa penati na Ricardo Rodriguez.


Michezo ya Marudiano kwa timu hizo itachezwa Novemba 12 na washindi wa jumla watafuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia.

No comments