SAID NDEMLA KUTIMKIA NCHINI SWEDEN

Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza rasmi kuwa mchezaji wake Hamis  Said Juma (Ndemla) amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Sweden.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi kwa vyombo vya Habari inaeleza kwamba Ndemla amepata nafasi hiyo katika klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Ndemla atakuwa katika majaribio hayo kwa siku 14 na anataraji kuondoka Sweden hapo kesho tayari kwa majaribio hayo.

Klabu ya Simba inaamini Ndemla atafanya vizuri na kufuzu katika majaribio hayo,na kama itakuwa tofauti na hivyo basi mchezaji huyo ataendelea kuwepo katika klabu ya Simba.

Endapo kama Ndemla atafanikiwa kufudhu kwenye majaribio hayo basi ataungana na mtanzania mwenzake Thomas Ulimwengu anaekipiga katika klabu hiyo.

No comments