KISA MASHABIKI,NSAJIGWA ATOLEWA NA POLISI UWANJANI
Na,Said Ally
Kocha msaidizi wa timu soka ya Yanga,Shadrack Nsajigwa jana alijikuta kuwa katika wakati mkugu baada ya pambano la watani wa jadi Simba na Yanga kumalizika kwa kikosi chake kufungwa kwa jumla ya bao 1-0.
Nsajigwa alikuwa na wakati mgumu baada ya dakika 90 za mchezo huo kukamilika kutoka na baadhi ya mashabiki wa Yanga kuanza kumtolea lugha ya matusi wakitaka kocha huyo ajiuzulu nafasi yake ya ukocha wakidai hana mbinu za ufundishaji.
MWANDIKE BLOG,ilishuhudia baadhi ya mashabiki hao waliopandwa na jazba wakimsubiri Nsajigwa nje ya uwanja na wengine wakiwa nje ya chumba walichokuwa wachezaji wa Yanga wakimsubiri kwa lengo la kumpa shinikizo la kujiuzulu.
"Huyu sio kocha wa kuifundisha Yanga, kwanza tunajua yeye sio shabiki wa Yanga,utakumbuka yeye ndie aliyehusika kutoa penati tatu wakati Simba anatufunga goli tano,sisi tunaomba atuchie timu yetu yeye aende akafundishe timu nyingine hatumtaki"alisikika mmoja wa mashabiki wa Yanga.
Hata hivyo jeshi la Polis lilazimika kumlinda Nsajigwa hadi kwenye basi la timu wakati alipokuwa anatoka vyumbani baada ya jeshi hilo kubaini kuwa hali ya baadhi ya mashabiki haikuwa nzuri kwani wengi wao walikuwa na taharuki ya kutaka kumvamia kocha huyo.

Post a Comment