KAULI YA MATOLA BAADA YA MECHI YA SIMBA

Na Mwandishi Wetu
Kocha Mkuu wa Lipuli Fc Suleiman Matola amesema kwamba yeye hajauza mechi kama ilivyokuwa inaelezwa awali, hii imekuja baada ya timu yake ya Lipuli Fc kutoka sare ya bao 1-1 na timu ya Simba.

Timu ya Lipuli fc ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa mchezaji wake mahiri Adam Salamba kunako dakika ya 31 ya mchezo huku Simba ikiwalazimu kusubiri hadi dakika ya 65 kusawazisha bao hilo kupitia Laudit Mavugo.

"Unajua inapotokea mechi sisi na Simba,sisi ambao tumekulia kwenye familia ya Simba tunaonekana kwamba tunauza mechi kwa Simba,kwa hiyo maneno yalikuwa mengi sana,ndio maana niliamua kuongea na wachezaji wangu kwa sababu nilichafuliwa kwa kuambiwa nimeuza mechi"alisema Matola wakati akihojiwa na Azam TV.

Aidha kocha huyo mnamo dakika ya 45 alionekana akijibizana na benchi lake la ufundi na alipoulizwa alijibu kwamba meneja wake alimuingilia katika kazi yake ikiwa yeye ndo boss Mkuu wa benchi la ufundi.

Kwa matokeo hayo Simba imeendelea kuwa kileleni katika msimamo wa ligi kwa alama  59  baada ya kucheza mechi 25 huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Yanga yenye alama 47 wakicheza michezo 22 na Lipuli Fc kwa upande wao inakamata nafasi ya saba kwa ala 32 wakishuka dimbani mara 26.

No comments