AKILIMALI ATUMA SALAMU KWA SIMBA
Na Said Ally
Katibu wa Baraza la wazee ndani ya klabu ya Yanga,Ibrahim Akilimali amesema kwamba kutinga kwao katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika ni salamu tosha kwa watani wao wa jadi Simba kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara.
Akilimali amesema kwamba baada ya jana Yanga kufanikiwa kuingia katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho kwa wastani wa ushindi wa jumla 2-1 dhidi ya Wolaitta Dicha ya Ethiopia kunaipa nguvu na hamasa kubwa hasa kuelekea kwenye mchezo huo utakaopigwa April 29 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Alisema kwamba morali waliyonayo baada ya matokeo hayo anaamini mechi yao ya April 29 watavunja rekodi ya Simba ya kutofungwa katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu.
Yanga imefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika licha ya kufungwa kwa bao 1-0,hii inatokana na mtaji mzuri wa ushindi wa mabao 2-0 walioupata hapa nyumbani.

Post a Comment