YANGA WAONGEZA WATU WA KAZI HUKO NCHINI ETHIOPIA

Katika kuonyesha kuwa Yanga imedhamiria kuingia hatua ya Makundi kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika,imeamua kuongeza baadhi ya viongozi wa klabu hiyo kwenda kuongeza nguvu nchini Ethiopia.

Mwenyekiti wa mashindano ndani ya klabu ya Yanga Hussein Nyika ameiambia MWANDIKE.BLOG kuwa yeye na baadhi ya viongoni wengine wameondoka Ethiopia kuungana na wenzao waliotangulia awali.

Alisema kwamba dhamira yao ni kwenda kuwapa hamasa ya kutosha wachezaji ili kuhakikisha wanachomoza na ushindi kwenye mpambano huo utakaoamua timu itakayoingia kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Yanga inataraji kushuka dimbani hapo kesho kumenyana na Wolaita Dicha,mchezo unaotarajiwa kupigwa huko nchini Ethiopia ambapo mechi ya awali Yanga ilichomoza na ushindi wa mabao 2-0.

No comments