TFF YATAJA VIINGILIO VYA MECHI YA SIMBA NA YANGA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara(VPL) msimu wa 2017/2018 kati ya Simba na Yanga utakaochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Katika mchezo huo namba 178 utakaofanyika saa 10 jioni Kiingilio cha chini kitakuwa shilingi Elfu Saba(7,000) wakati kiingilio cha juu kitakuwa shilingi Elfu Thelathini.
Jukwaa la VIP A itakuwa shilingi Elfu Thelathini (30,000),VIP B na C shilingi Elfu Ishirini (20,000) na Upande wa Mzunguko kwenye viti vya rangi ya Chungwa,Bluu na Kijani itakuwa shilingi Elfu Saba (7,000)
Tiketi tayari zimeanza kupatikana kuanzia sasa kupitia Selcom.
Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and 

No comments