VPL KUENDELEA LEO HII

Ligi kuu ya Tanzania bara inataraji kuendelea leo katika viwanja vinne tofauti hapa nchini.

Lipuli FC watakuwa nyumbani kuwakaribisha walima alizeti Singida United katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.

Mwadui FC itaialika Stand United kwenye uwanja wa Mwadui Complex,wakati kwenye uwanja wa CCM Kirumba wanalizombe wa Majimaji watakuwa wageni wa Mbao FC ya Ilemela mkoani Mwanza.

Mechi nyingine itakayochezwa leo hii ni kati ya Azam FC dhidi ya Njombe,mchezo unaotarajiwa kupigwa kunako mishale ya saa moja kamili usiku kwenye uwanja wa Azam Complex jijini Dar es salaam.

No comments