DROO YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA KUPANGWA KESHO

Droo ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika inatarajiwa kupangwa rasmi hapo kesho huko Cairo nchini Misri kuanzia mishale ya saa nane mchana kwa saa za hapa nyumbani.

Timu 16 zimefanikiwa kutinga katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

Kuongezeka kwa timu msimu huu kumeleta faida kwa timu za ukanda wa Afrika Mashariki baada timu nyingi za ukanda huo kama Gor Mahia ya Kenya,Rayon Sports ya Rwanda nazo zikifanikiwa kuingia kwenye hatua hiyo ya makundi.

Tanzania inawakilishwa na timu ya Yanga kwenye michuano hiyo kwa ngazi ya vilabu baada ya kuiondosha Wolaitta Dicha ya Ethiopia kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.

No comments