ANDIKO LA MASAU BWIRE WAKATI YANGA IKITARAJI KUIVAA WOLAITA DICHA

Klabu ya Yanga, mwakilishi pekee wa nchi katika mashindano ya Kimataifa, leo yuko uwanjani, Ethiopia, mchezo wa marudiano utakaoamua, asonge mbele au safari iishie hapo!

Watanzani, Yanga ni ya Tanzania, sisi ni Watanzania, kila mmoja kwa dini na imani yake aiombee timu yetu  hii isonge mbele.

Tuache mambo ya kizamani, tuwe wa sasa kwa usasa wa sasa katika dunia ya sasa, tupende chetu.

Kuiombea Yanga kutolewa mashindanoni ni kukosa uzalendo na kuwanyima fursa si tu Yanga bali Watanzania wote, nawe ukiwa miongoni, unajinyima fursa!

Yanga ikisonga mbele faida ni nyingi mno ambazo sina sababu kuzitaja, kwani najua mnazijua!

Hivi utafaidika nini Waethiopia wakisonga mbele au utapata hasara gani Watanzania wenzako wakisonga mbele?

Tuache mambo ya zamani jamani, hayo tayari ni zilipindwa, yabaki tu historia, twende na usasa wa sasa katika ushabiki wetu.

Vikumbo tupigane, tupapase na mpapaswe katika ligi yetu ya ndani, suala la Kimataifa tuwe kitu kimoja, tukipende cha kwetu, tukishangilie, tukiombee ushindi!

Eeeee Mungu wa Mbinguni, tupatie ushindi Watanzania, Yanga yetu isonge mbele!

Masau Bwire-Mzalendo

No comments