POST YA JOKATE BAADA YA NDOA YA ALLY KIBA YAWA GUMZO


Gumzo kwa sasa katika mitandao ya kijamii ni kuhusiana na ndoa ya msanii wa bongo Fleva Ally Kiba ambae siku ya leo amefunga ndoa na mkewe Bi.Amina Ahmed mjini Mombasa nchini Kenya.

Wadau mbalimbali wameendelea kumpongeza Ally Kiba kwa jambo jema ambalo amelifanya la kuamua kufunga ndoa na mkewe huyo kutoka nchini Kenya kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo facebook,instagram nk.
Lakini pia wadau hao baadhi yao wameonyesha kumkebehi Jokate Mwegelo anaesadikiwa kuwa awali alikuwa na mahusiano na Ally Kiba,kutokana na kitendo cha msanii huyo kumuacha yeye na kwenda kuamua kuoa mke mwingine.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Jokate aliandika maneno matatu yaliyosemeka "LOL"huku akiweka picha inayoenekana kama ana uzuni jambo ambalo limepokelewa tofauti na baadhi ya watumiaji wa mtandao huo.
Hata hivyo baadhi yao wamekuwa wakimpa pole mwanadada huyo wakimsihi atulie kwani wana imani atapata mume bora.


No comments