ZFA YABEBESHWA ZIGO LA LAWAMA BAADA YA KARUME BOYS KUFUNGIWA

Na,Sleiman Ussi,Zanzibar
Wadau wa soka visiwani Zanzibar wamekilaumu chama cha soka cha ZFA wakisema kwamba wao ndio chanzo kikubwa za kuzoletesha maendeleo ya soka visiwani humo.

Hayo yameelezwa baada ya timu ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 Karume Boys kufungiwa mwaka mmoja na kupigwa faini ya dola 15,000 kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozidi umri katika mashindano ya CECAFA yanayoendelea nchini Burundi.

Mmoja wa wadau hao aliyejitambulisha kwa jina la Amir Rashidi "Mero"alisema kwamba ZFA wanapaswa kulaumiwa kwa sababu imefikia hatua hadi kamati ya Central Zanzibar haijui aliyehusika na uchaguzi wa wachezaji wa timu hiyo.

Alisema kwamba Zanzibar kuna vijana wengi ambao wanajua vizuri kucheza mpira lakini uchaguzi wa kikosi hicho ambacho kilichaguliwa kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo ya vijana,ulifanywa kwa upendeleo.


No comments