YANGA YAIFUATA WOLAITA DICHA BILA AJIBU

Na Said Ally
Kikosi cha timu ya soka ya Yanga leo hii kimesafiri kuelekea nchini Ethiopia kuwafuata Wolaita Dicha kwa ajili ya mchezo wa pili wa kombe la shirikisho barani Afrika utakaopigwa siku ya jumatano.

Katika msafara huo Yanga haikuambatana na mchezaji Ibrahim Ajibu ambae inataarifiwa anasumbuliwa na Malaria.

Mbali na Ajibu wachezaji wengine walioshindwa kusafiri na timu ni pamoja na Ramadhani Kabwili ambae yeye yupo kwenye kikosi cha timu ya vijana Ngorongoro Heroes kinachojiandaa na mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa vijana dhidi ya DR Congo.

Wengine waliosalia kutokana na kuwa majeruhi ni pamoja na Donald Ngoma,Amis Tambwe huku pia  kinda Said Mussa nae yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya viajana.

Wachezaji waliosafiri ni pamoja na

Magolikipa
1.Youthe Rostand
2.Beno Kakolanya

Mabeki
1.Juma Abdul
2.Hassan Kessy
3.Haji Mwinyi
4.Kelvin Yondani
5.Nadr Haroub
6.Abdalah Shaibu
7.Gadiel Michael

Viungo
1.Said Makapu
2.Raphael Daud
3.Pius Buswita
4.Thabani Kamusoko
5.Papy Tshishimbi
6.Yusuf Mhilu
7.Geofrey Mwashiuya
8.Emmanuel Martine

Washambuliaji
1.Juma Mahadhi
2.Obrey Chirwa
3.Yohana Mkomola

No comments