YANGA YAPANGWA KUNDI D KATIKA MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA

Yanga imepangwa katika kundi D kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika kufuatia droo iliyofanyika leo hii Cairo nchini Misri.

Miongoni mwa timu ambazo zimepangwa kundi D ni pamoja na Rayon Sport ya nchini Rwanda,U.S.M Alger ya Algeria pamoja na Gor Mahia ya nchini Kenya.

Kundi A lina timu za Asec Mimosas,Raja Club Athletic,AS Vita Club na Aduana Stars FC.

Kundi B lina timu ya RS Berkane,El Masry Club,Uniao Desportivo na Al Hilal

Kundi C kuna timu ya Enyimba,Williamsville,Cara Brazaville na Djoliba AC.

Yanga ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo endapo itajipanga vizuri,hii inatokana na timu ambazo amepangwa nazo katika kundi D kuzifahamu vizuri kwani katika kundi hilo timu tatu zinatoka kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

No comments