RAIS MAGUFULI AIRUDISHA URAIANI FAMILIA YA BABU SEYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,John Pombe Magufuli leo hii siku ya jumamosi ametangaza msamaha kwa familia ya Babu Seya waliokuwa wamefungwa kifungo cha maisha.

Rais Magufuli ametoa msamaha huo wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Uhuru yaliyofanyika mkoani Dodoma.

Familia hiyo ya Babu Seya ilihukumiwa kifungo cha maisha na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu mwaka 2004 baada ya kukutwa na hatia ya kunajisi na kulawiti watoto wadogo.

No comments