TFF WASEMA JERY MURO ANA HAKI YA KUKATA RUFAA MBELE YA KAMATI NYINGINE


Kamati ya maadili ya TFF ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Wakili Wilson Ogunde mara baada ya kuweza kumfungia mkuu wa mawasiliano wa klabu ya Yanga Jerry Muro mwaka mmoja kutojihusisha na masuala ya soka pamoja na kutozwa faini ya Sh. Milioni 3,hii leo uongozi wa shirikisho hilo la mpira wa miguu hapa nchini umesema kwamba kwa upande wake umeridhika na adhabu hiyo iliyotolewa na kamati husika

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba licha ya kosa moja kutomuweka hatiani lkn wao wamekubaliana na maamuzi hayo na kwa sasa kamati husika inafanya jitihada za kuandaa hukumu yake ili aweze kufahamu maamuzi ya kamati ya maadili

Aidha amesema kwamba endapo kama Jerry Muro hataridhika na maamuzi hayo basi anapaswa kukata rufaa kwani bado ana haki ya kusikilizwa na kamati nyingine

Hata hivyo Jerry Muro amesema kwamba kwa sasa yeye ataendelea kufanya kazi ndani ya Yanga hadi hapo viongozi wa timu hiyo watakapomsimamisha kazi

Muro amedai kua yeye ameajiliwa na Yanga wala sio TFF,hivyo hatua ambayo imefanywa na kamati ya maadili ya TFF haikua sahihi ksb waliopaswa kuhukumiwa ni Yanga ambao ndio wamemuajiri

No comments