HATMA YA SHIZA RAMADHANI KICHUYA JUU YA KUJIUNGA NA SIMBA KUJULIKANA HAPO KESHO


Wakata miwa wa Manungu Turiani mkoani Morogoro timu ya Mtibwa Sugar,wamesema kwamba hapo kesho wanataraji kulitolea ufafanuzi swala la mchezaji Shiza Ramadhani Kichuya juu ya kujiunga kwake na klabu ya Simba ama kusalia kunako wakata miwa hao wa Manungu

Msemaji wa timu hiyo Tobiasi Kifaru amesema kwamba kwa sasa yeye yupo jijini Dar es salaam pamoja na mchezaji huyo hivyo kwa leo hatuzungumza chochote ambacho kinahusiana na mchezaji huyo hadi hapo kesho atakapoweka mambo hadharani

Amesema kwamba Kichuya ni moja ya wachezaji anaehitajika na vilabu vingi vya hapa nyumbani kutokana na uwezo wake ambao ameuonyesha kwenye michezo ya ligi kuu pia hata wao bado wana nia ya kuendelea na huyo mchezaji endapo kama atakua na nia ya kusalia katika klabu hiyo

Hata hivyo kwa sasa kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo ambae amebakiza mkataba wa mwaka mmoja msimu ujao akaonekana kwenye kikosi cha wekundu wa msimbazi Simba kufuatia mazungumzo ambayo yanaendelea baina ya pande hizo huku mchezaji akiwa tayari kujiunga na klabu hiyo ispokua kwa sasa kinachokwamisha ni kuhusiana na mkataba alio nao na Mtibwa Sugar

No comments