SALUMU MAYANGA ARITHI MIKOBA YA MECK MEXME KATIKA KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR


Mara baada ya Meck Mexme kusaini kandarasi ya mwaka mmoja kuifundisha timu ya Kagera Sugar,hii leo ungozi wa timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mkoani Morogoro umemtangaza rasmi Salum Mayanga kua ndie kocha mpya wa timu hiyo inayotaraji kuanza mazoezi siku ya jumatatu jijini Dae es salaam

Akiongea na Saidallymwandike.blogsport kwa njia ya simu,msemaji wa timu hiyo Tobiasi Kifaru amesema kwamba wamechukua jukumu la kumkabizi mikoba Mayanga ambae alikua anaifundisha timu ya Tanzania Prisons msimu uliopita kwa sababu yeye ni mwajiliwa wa kampuni hiyo inayoimiliki Mtibwa Sugar kwa miaka 20

Aidha Kifaru amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo baada ya idadi kubwa ya wachezaji wake kuondoka katika vilabu vingine ambapo amesema kwamba hilo halina shida kwao kwani Mtibwa Sugar ni sawa na chuo cha kukuza vipaji hivyo wategemee kuwaona wachezaji wengine wapya ambao watakua na viwango bora zaidi.

No comments