KMC YAKABIZIWA KWA WANANCHI WA KINONDONI

 
Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniphace Jakobo ameikabidhi rasmi timu ya manispaa ya hiyo KMC kwa wananchi ili kuiwezesha timu hiyo inapata nafasi ya kupanda daraja na kushiriki katika ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao

Akizungumza katika kikao na wadau wa soka wa manispaa hiyo Jakobo amesema kwamba lengo lake ni kuona wananchi wa manispaa hiyo wanahusika kwenye changamoto za timu hiyo kwa kuweza kufanya shughuli mbalimbali ambazo zitakua na tija za kuisaidia timu iweze kufanya vizuri kwenye mechi mbalimbali za ligi daraja la kwanza

No comments