KOCHA MSAIDIZI WA SERENGETI BOYS AWATOA HOFU WATANZANIA JUU YA UMRI WA WACHEZAJI WA TIMU HIYO KWENYE USHIRIKI WA MICHUANO YA KUSAKA TIKETI YA KUFUZU KWA FAINALI ZA VIJANA


Kocha msaidi wa timu ya Serengeti boys,Sebastian Nkoma amewataka watanzania kuondoa hofu juu ya timu hiyo kuhusiana na swala la umri wa wachezaji wa kikosi cha timu kinachoendelea kufanya vizuri katika michezo yake mbalimbali

Akiongea na Saidallymwandike.blogsport,Nkoma amesema kwamba wachezaji wote 24 wa Sengeti Boys wanastahili kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa kila mmoja ameshafanyiwa vipimo vya kutambua umli na wahusika wakuu wa jambo hilo

Amesema kwamba kwa sasa kutokana na mfumo wa uendeshaji wa mpira wa miguu ulivyobadilika itakua jambo gumu kumchezesha mchezaji ambae hana sifa ya kushiriki michuano kwenye michuano ambao wanashiriki ya kuwania kufuzu kwa fainali za vijana za Afrika

Mara baada ya kufanikiwa kuiondosha timu ya Shelisheli kwa jumla ya bao 9-0 sasa Serengeti Boys inajiandaa na mchezo wao unaofuta dhidi ya Afrika ya Kusini ambao wataanzia ugenini

No comments