SAID MORAD AKANUSHA TAARIFA ZA KUJIUNGA NA SIMBA


Mchezaji aliyemaliza muda wake katika klabu ya Azam ya jijini Dar es salaam,Said Morad amekanusha taarifa za kujiunga na klabu ya Simba kama baadhi ya mitandao mbalimbali imekua ikilipoti juu ya kujiunga kwake

Akiongea na Saidallymwandike.blogsport,Morad amesema kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani hakuna mazungumzo ambayo waliyokubaliana na timu hiyo yenye makazi yake mitaa ya Msimbazi ya kusaini mkataba

Hata hivyo kumekua na taarifa kwamba huenda mchezaji huyo msimu ujao akaitumikia timu ya Simba hii inatokana na baadhi ya viongozi wa timu hiyo kuhitaji huduma za mchezaji huyo

No comments