MARA BAADA KUFUNGIWA KUTOJIHUSISHA NA SOKA KWA MWAKA MMOJA,JERRY MURO AWAAMBIA TFF WANAKIMBIA MBIO PASIPO KUIJUA NJIA


Kamati ya maadili ya TFF imemfungia mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga,Jerry Muro mwaka mmoja kutojihusisha na maswala ya soka pamoja na kulipa faini ya shilingi milioni tatu kwa kosa la kudharau maamuzi ya kamati ya nidhamu ya TFF kwa kitendo chake cha kukaidi kulipa kiasi cha Shilingi milioni tano baada ya kutakiwa kulipa na kamati hiyo kwa kufanya makosa kwa TFF,pamoja na kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea kwenye mchezo wa kombe la shirikisho barania Afrika dhidi ya TP MAZEMBE ambapo katika shitaka hilo alilopigwa faini ya kulipa milioni tatu,Jerry anadaiwa kuwashawishi mashabiki wa Yanga kuwafanyia vurugu mashabiki wa Simba katika pambano hilo lililomalizika kwa Yanga kufungwa bao 1-0

Hata hivyo mara baada ya hatua hiyo,Jerry Muro amesema kwamba TFF ni kama wanakimbia mbio ili hali njia hawaijui,inamaana kutokana na kauli hiyo inaonyesha Muro anajiandaa kukata rufaa kuhusiana na kutokubaliana na maamuzi hayo

No comments