NAMPALY'S MEND ASAJILIWA NA LEICETER CITY


Timu ya  Leiceter ya nchini England imekamilisha usajili wa midfield wa timu ya Nice ya nchini Ufaransa,Nampaly's Mend kwa kuweza kumpa kandarasi ya miaka minne ambayo ataitumikia mabingwa hao wa ligi kuu ya England.


Hata hivyo, Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 hajawahi kuitwa katika kikosi cha taifa cha Ufaransa.

Hadi tulipochapisha habari hizi haikuwa imebainika mkataba huo ni wa kitita cha pesa ngapi.
Mendy alijiunga na Nice mwaka wa 2013 akitokea klabu ya Monaco alikoichezea katika mechi 110 za ligi ya daraja ya juu Ligue 1 katika misimu 3.
Mendy ni mchezaji wa tatu kujiunga na Leicester baada ya kipa Ron-Robert Zielerand na mlinzi Luis Hernandez.

No comments