PAULO NONGA MBIONI KUJIUNGA NA MOJA YA KLABU YA LIGI KUU YA TANZANIA BARA


Mchezaji wa timu ya Yanga,Paulo Nonga amekiri kuwepo katika hatua nzuri na moja ya vilabu vya ligi kuu ya Tanzania bara kwa ajili ya kuitumikia katika msimu ujao

Akiongea na Saidallymwandike.blogsport,Nonga amesema kwamba kwa sasa mazungumzo baina ya timu hiyo ambayo amekataa kuitaja yanaendelea vizuri na viongozi wa Yanga hivyo huenda itakapofika siku ya jumatano itafahamika rasmi wapi aendako

Amesema kwamba anaupongeza uongozi wa Yanga kwa namna jinsi walivyoweza kumkubalia ombi lake la kutaka kuuzwa katika klabu nyingine mara baada ya kuona hana nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha timu hiyo kutokana kuwepo na wachezaji wengi ambao wamemzidi kiwango kwenye nafasi yake anayocheza

Hata hivyo amesema kwamba mazungumzo ambayo yanaendelea ni ya kuuzwa moja kwa moja na si kwa mkopo kama inavyodaiwa na baadhi ya watu

No comments