MENEJA WA MBWANA SAMATA AWEKA BAYANA KUHUSIANA NA TAARIFA ZA SAMATA KUJIUNGA NA AS ROMA YA ITALIA


Meneja wa mchezaji Mbwana Samata,Jamali Kisongo amesema kwamba hakuna mazungumzo yeyote ambayo yanaendelea na viongozi wa timu ya AS ROMA ya nchini Italia juu ya mchezaji huyo kujiunga na klabu hiyo

Akiongea na Saidallymwandike.blogsport,Kasongo amesema kwamba taarifa ambazo zipo katika baadhi ya mitandao si za kweli kwani hakuna mawasiliano baina ya pande hizo

Amesema kwamba leo hii amezungumza na Samata pamoja na baadhi ya viongozi wa timu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji na wamemwambia hakuna taarifa hizo zinazohusiana na usajili wa mchezaji huyo

Hata hivyo amesema kwamba endapo kama timu hiyo ya Italia itakua na nia ya kutaka kumsajili basi ni vyema wakawasiliana na viongozi husika kwani kwa mujibu wa taarifa yake Genk hawatakua na kikwazo juu ya swala zima la kuuzwa kwa mchezaji huyo ambae kwa sasa ni moja ya wachezaji wa kutegemewa kwa timu ya KRC GENK

No comments