NIYONZIMA NA WAWA WAWEKWA PEMBENI KATIKA TUZO ZA MCHEZAJI BORA WA KIGENI
Hafla ya kukabidhi tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016 itafanyika Julai 17 mwaka huu.
Jumla ya tuzo 13 za Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa katika hafla hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam, na kuratibiwa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Wachezaji ambao wamependekezwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa ligi ni Shiza Kichuya [MTIBWA SUGAR] Juma Abdul [YANGA] na Mohamed Hussein [SIMBA]
Kwa upande wa kipa bora ni Aishi Manula [AZAM] Beno Kakolanya [PRISONS] na Deogratius Munishi [YANGA]
Kocha bora wapo Hans Pluijum [YANGA] Mecky Mexime [MTIBWA SUGAR] na Salum Maynga [TANZANIA PRISONS]
Pia waliopendekezwa kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi ni Farid Musa [AZAM] Mohamed Hussein [SIMBA] Mzamiru Yasini [MTIBWA SUGAR] na Shiza Kichuya [MTIBWA SUGAR]
Walioingia kwenye orodha ya tuzo ya mchezaji bora wa kigeni ni Dornad Ngoma [YANGA] Thabani Kamusokao [YANGA] na Vicent Agban [SIMBA]
Kwa upande wa waamuzi bora ni pamoja na Anthony Kayombo,Ngole Mwangole na Rajabu Mrope.
Post a Comment