BAADHI YA MASHABIKI WA SIMBA WAMKATAA DEWJI
Baadhi ya mashabiki wa timu ya Simba wamepingana na hatua ambazo zinataka kuchukuliwa na Bilionea kijana, Mohammed Dewji juu ya mpango wake wa kutaka kununua hisa za asilimia 51 kwenye klabu hiyo
Mmoja wa mashabiki hao aliyejitambulisha kama Mgeni Ramadhani jina maarufu dogo Macho amesema kwamba,Mohamed Dewji hastahili kupewa timu ya Simba ksb awali alipokua anaidhamini timu hiyo alishindwa kuiendesha timu hiyo kwa weledi na kupelekea kuikimbia Simba wakati Simba inacheza ligi ndogo mkoani Morogoro
Amesema kwamba Dewji alishindwa kutimiza maagizo yake amabayo aliyatoa kwa wanachama ikiwa ni pamoja na swala lake la kujenga uwanja na vitega uchumi kwa maendeleo ya Simba
Hata hivyo amewatahadharisha wanachama hai wa Simba kuelekea kwenye mkutano mkuu wa kesho kua makini na jambo hilo kwani wasipokua makini kutaleta athari kubwa kwa timu hiyo hapo mbeleni
Nae mshabiki mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Tifa Ramadhani Simba,amesema kwamba kwa upande wake nae pia anapingana na matakwa ya Mohamed Dewji juu ya kutaka kununua hisa za asilimia 51 ndani ya klabu hiyo kwani hakuna utaratibu mzuri ambao umetumika kwa ajili ya kumpata mwekezaji sahihi.
Post a Comment