MOHAMED DEWJI ATAWALA KATIKA MKUTANO MKUU WA SIMBA
Mkutano mkuu wa wanachama wa klabu ya Simba ambao umefanyika leo umemalizika baada ya uongozi wa klabu hiyo kuwasilisha agenda tisa na kumi ni ya kufunga mkutano ambapo kikubwa zaidi kilichokua gumzo kwenye mkutano huo ni juu idadi kubwa ya wanachama kuutaka uongozi umkabidhi timu bilionea kijana Mohamed Dewji.
Agenda ya kujadili swa la Dewji ya kutaka kununua hisa asilimia 51 ilikua ni agenda ya tisa ambayo inasema juu ya taarifa ya kamati ya maboresho ya mfumo wa uendeshaji ambapo idadi kubwa ya wanacha wengi wamekua wakiisubiria hiyo huku wakikosa usikivu wakati agenda nyingine zilivyokua zinazungumzwa
Baadhi ya wanachama kwa muda wote walikua wanataja jina la Mohamedi Dewji katika harakati za kukubaliana na maamuzi yake ambayo anayoyataka kuyafanya ndani ya klabu ya Simba ya kununua hisa za asilimia 51 kwa shilingi bilioni 20.
Hata hivyo wanachama wa klabu hiyo waliibua shangwe pale Raisi wa klabu Evansi Aveva aliposema kwa mara nyingine kwamba maoni yao ya kutaka kumkabidhi timu Dewji yatasikilizwa.
Agenda ambazo zimejadiliwa leo hii ni;
1;Uhakiki wa wanachama waliohudhuria
2;Kuthibisha agenda
3;Kusoma na kuthibitisha mukhtasari wa mkutano uliopita
4;Yatokanayo na kumbukumbu za mkutano uliopita
5;Hotuba ya Raisi na kupokea na kujadili taarifa kutoka kamati ya utendaji
6;Kuthibisha hesabu za fedha zilizokaguliwa za mwaka uliopita
7;Kuthibitisha taarifa za chombo cha ukaguzi na hatua zilizochukuliwa
8;Kuthibitisha bajeti ya mwaka unaofuata
9;Taarifa ya kamati ya maboresho ya mfumo wa uendeshaji
10;Kufunga mkutano
Post a Comment