SHEIKH SAID BADO MAKAMU MWENYEKITI TPLB
Bwana Said
Mohamed bado ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) baada ya
kuingia kwenye wadhifa huo katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 2013.
Nafasi hiyo ya
Bw. Mohamed ni kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji za TPLB, na aliipata kupitia
uchaguzi huo. Pia Makamu Mwenyekiti huyo ni Mwenyekiti wa klabu ya Azam FC
inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.
Bw. Mohamed
alikuwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Salim Said Bakhresa ambayo pia inamiliki pia
timu ya Azam FC kabla ya kustaafu Mei mwaka huu. Licha ya kustaafu ajira yake
ndani ya SSB, lakini Bw. Mohamed bado ni Mwenyekiti wa Azam FC.
Kwa mujibu wa
Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti wa TPLB pia ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo na
wanaendelea na majukumu yao kama kawaida.
Post a Comment