MAAGIZO KWA KLABU ZA LIGI KUU, LIGI DARAJA LA KWANZA
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameziasa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutimiza masharti ya kupata vibali vya kuishi na kufanya kazi Tanzania kwa wachezaji na wataalamu wa kigeni wakiwamo makocha na madaktari kabla ya kuingia nao kandarasi za ajira.
Masharti hayo ni vibali vya kufanya kazi nchini, visa za kuishi nchini, vibali vya kucheza mpira wa miguu nchini, vibali vya kufundisha mpira na vibali vya watalaamu wengine kama madaktari na hayo ni kwa mujibu wa Idara ya Uhamiaji na mamlaka nyingine za serikali na kanuni za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini ,TFF.
“Mchezaji au mtaalamu ye yote anapokuja nchini na kuanza mazoezi na timu yo yote anachukuliwa yuko kazini. Tusingependa watu wapate usumbufu. Kama Katibu Mkuu na mtendaji mkuu, nimepata maelekezo kutoka mamlaka zinazohusika kuwa nifuatiulie kuwa TFF kamamratibu mkuu wa mchezo wa mpira wa miguu ina jukumu la kuhakikisha wanachama wake wanafuata taratibu.natakiwa kufuatilia,” amesema Selestine.
“Vilabu vihakikishe vyeti vya taaluma vinawasilishwa TFF kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kutiliana kandarasi na wachezaji au walimu. . Ni vema wakafanya uratatibu wa kuhakiki Hii itaviepusha vilabu na gharama za fidia au kesi za madai endapo mamlaka za serikali au za mpira zitasita kumruhusu mhusika kufanya kazi nchini,” amesema.
Vilevile Katibu Mkuu wa TFF amezitaka klabu kumalizana na wachezaji na wataalamu zinaoachana nao kabla ya kufikiria kuingiza wapya.TFF tayari ina barua kadhaa za madai ya wachezaji na watumishi wa vilabu waliomaliza au kukatishwa mikataba yao bila kulipwa mafao yao.TFF inawataka kumaliza masuala haya ili kuweza kujikita vema katika kupanga safu zao kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi.
Wakati huohuo, huo huo TFF imeagiza klabu kuendelea na usajili kabla ya Agosti 6, 2016 ambayo itakuwa siku ya mwisho na kwamba hakutakuwa na muda wa kuongezwa kwa klabu ambayo itashindwa kukamilisha usajili kwa wakati.
Post a Comment