MKWASA AITA NYOTA 24 STARS
Kocha Mkuu timu
ya Mpira Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa ameita kikosi cha
wachezaji 24 watakaoanza kambi ya awali kuajindaa na mchezo dhidi ya Nigeria
utakaofanyika Lagos, Septemba 2, 2016.
Kwa mujibu wa
Mkwasa, timu hiyo itaingia kambini Agosti 1, 2016 na itadumu kwa siku tano tu
kabla ya kuvunjwa na kuitwa tena mwishoni mwa mwezi Agosti, 2016 kujiandaa na
kambi ya mwisho na moja kwa moja itakuwa ni kwa ajili ya safari kwenda Nigeria.
Katika kikosi
hicho, Mkwasa hajaita nyota wa kimataifa akiwamo Nahodha, Mbwana Samatta wa FC
Genk ya Ubelgiji na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo (DRC) kwa sababu ya majukumu waliyonayo kwenye klabu zao kwa sasa.
Kadhalika,
nyota hao wataungana na wenzao nchini Nigeria kwa kuwa mchezo huo upo kwenye
kalenda ya CAF na ni wa mashindano. Mchezo huO ambao ni wa kukamilisha ratiba, Mkwasa
amesema utakuwa mgumu kwani Nigeria wamebadili benchi la ufundi hivyo kila timu
inaungalia mchezo huu kwa jicho la pekee.
Wachezaji
walioitwa ni:
Makipa:
Deogratius
Munishi
Aishi Manula
Benny
Kakolanya
Mebeki:
Kelvin Yondani
Aggrey Morris
Oscar Joshua
Mohamed Husein
‘Tshabalala’
Juma Abdul
Erasto Nyoni
Viungo:
Himid Mao
Mohamed
Ibrahim
Shiza Kichuya
Jonas Mkude
Ibrahim Jeba
Mwinyi
Kazimoto
Farid Mussa
Juma Mahadhi
Hassan Kabunda
Washambuliaji:
Simon Msuva
Joseph Mahundi
Jamal Mnyate
Ibrahim Ajib
John Bocco
Jeremia Juma
Post a Comment