INFANTINO AMSIFU MALINZI
Rais wa
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino amemsifu
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuwa ni miongoni mwa
viongozi wa vyama vya soka duniani walioamua kuendesha soka kwa weledi kutokana
na kuratibu mafunzo mbalimbali kwa makocha na waamuzi.
Salamu za
Infantino zimetolewa na Msimamizi Mkuu wa kozi ya waamuzi nchini, Carlos
Henrique kutoka Afrika Kusini akisema, “Infantino ana ripoti zote ya namna
mpira wa miguu unavyoendeshwa duniani. Anasifu Tanzania kwa namna mnavyopiga hatua. Ana ripoti idadi ya
makocha walivyokuwa wachache na sasa mna makocha wengine wako kwenye kozi.
“Mbali ya
makocha, leo tuko nanyi waamuzi, ni hatua kubwa ambayo Rais Infantino amemsifu
Rais wa TFF, Bwana Malinzi,” alisema Henrique.
Henrigue
aliyeka waamuzi hao kujikita zaidi kusoma namna sheria 17 za mpira wa miguu
zilivyoboreshwa kwa kuondoa zaidi ya maneno 1,000 ili kuja kusimamia vema
michezo wa soka huku akiwataka kuwa mahiri wakati wote. Henrique anafanya kazi
hiyo kwa kushirikiana na Mark Mzengo kutoka Malawi, Felix Tangawarima wa
Zimbabwe na Gladys Onyago kutoka Kenya.
Kozi za
Waamuzi wa Mpira wa Miguu wa Tanzania sasa ilianza jana Julai 25, 2016 kwa waamuzi wenye Beji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) na waaamuzi waandamizi
wanaotarajiwa kuveshwa beji hizo kwa majina yao kupendekezwa FIFA kama watapata
matokeo mazuri kwenye kozi inayoendelea.
Kozi ilianza
kwa ratiba ya waamuzi wote kuchukuliwa vipimo (physical fitness test) kwa kila
mwamuzi chini ya wakufunzi hao kutoka FIFA. Baada ya vipimo, darasa la waamuzi
hao litaanza kwa nadharia na vitendo. Darasa hilo litafikia mwisho Julai 29,
2016 kabla ya kuanza darasa la waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
(VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) na
makamishna wa michezo kwa msimu wa 2016/2017.
Post a Comment